Haya yamesemwa na Hossein Simaei Saraf, Waziri wa Sayansi, Utafiti na Teknolojia wa Iran, alipohutubia maandamano ya kuunga mkono Palestina yaliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Tehran siku ya Jumatatu.
Amesema: “Tutawakaribisha kwa furaha na fahari yoyote profesa au mwanafunzi wa Kipalestina anayetaka kujiunga na kitivo au kuendeleza masomo yake katika vyuo vikuu vya Iran."
Tangu kuanza kwa vita mnamo Oktoba 7, 2023, mashambulizi ya anga ya Israeli yameharibu kabisa miundombinu ya vyuo vikuu vya Gaza. Taasisi mashuhuri zilizobomolewa kabisa ni kama vile Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Gaza, Chuo Kikuu cha Al-Azhar, Chuo Kikuu Huria cha Al-Quds, Chuo Kikuu cha Al-Israa, na Chuo Kikuu cha Al-Aqsa na Chuo cha Sayansi na Chuo Kikuu cha Palestina. Kwa mujibu wa Wizara ya Elimu ya Palestina, mashambulizi haya yamesababisha vifo vya wanafunzi wasiopungua 4,327 na walimu pamoja na watendaji 231, wakiwemo maprofesa wa vyuo vikuu 94 waliopoteza maisha.
Jamii ya kielimu imeita mashambulizi haya ya kimfumo kuwa ni "educide", yaani mauaji ya kimbari ya sekta ya elimu, ikieleza kuwa yanalenga kuvunja kabisa misingi ya elimu ya Gaza na kuangamiza mtaji wake wa kielimu. Uharibifu huu wa taasisi za elimu haumalizi tu ndoto za masomo za wanafunzi takriban 90,000, bali pia unavuruga mfumo mpana wa kijamii unaotegemea elimu kwa maendeleo na ustahimilivu.
Uvamizi wa utawala wa Kizayuni dhidi ya ardhi ya Palestina iliyowekewa mzingiro ulianza Oktoba 2023. Vita hivyo vya Israel vimesababisha vifo vya watu zaidi ya 50,900, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na karibu idadi yote ya wakazi wa Gaza kulazimika kuhama makazi yao ndani ya eneo hilo hilo.
Waziri huyo wa Iran amesema: “Kwa miongo kadhaa, utawala huu wa kihalifu unaoua watoto umeendelea kukiuka sheria zote za haki za binadamu, huku taasisi na mataifa yaliyosituka yakiendelea kulaani. Hata hivyo, uhalifu unaendelea."
Aidha amesema: “Kuendelea kwa uhalifu huu licha ya shutuma kubwa duniani kote kunaonyesha kuwa mifumo ya haki za binadamu siyo Madhubuti."
Amesema kuuawa kwa watoto na kutekelezwa kwa mauaji ya kimbari ni “miongoni mwa uhalifu wa chini kabisa” unaofanywa na utawala wa Israel na kuongeza kuwa , “uhalifu huu umeumiza hisia za ubinadamu, na huenda ni mara ya kwanza ambapo wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Marekani na Ulaya wanaandamana kila wiki kupinga dhulma hii kwa hiari yao.”
342/
Your Comment